• info@quantumarchitects.co.tz
  • +255-655-876543
  • 2023-05-17
  • Admin

 KIBALI CHA UJENZI (BUILDING PERMIT)

TARATIBU ZA KUPATA KIBALI CHA UJENZI (BUILDING PERMIT)

 1. KIBALI CHA UJENZI

Kulingana na Sheria ya Serikali za Mitaa Sura 288 (Urban Authorities) act (Cap. 288) (Development control Regulations, 2008, Mwongozo wa utoaji wa vibali vya ujenzi, 2018, si ruhusa kwa mtu yeyote kujenga au kuanza kujenga jengo bila ya :-

  •  Kutuma maombi kwa mamlaka ya mji husika.
  • Kuwasilisha michoro ya jengo na kumbukumbu husika.
  • Kupata kibali cha maandishi kinachoitwa Kibali cha Ujenzi.

2. KIBALI CHA AWALI:

  • Inashauriwa kupata kibali cha awali kabla ya kuomba kibali cha ujenzi.  Hivyo muendelezaji anatakiwa aandae mchoro wa awali (sketch plans scale) 1:00 1:200 akionyesha aina ya ujenzi atakaokusudia kufanya ili aweze kupata ridhaa ya kuendelea ha hatua za kuanzaa michoro ya mwisho.

Faida:

  • Kuokoa muda na gharama iwapo michoro ya mwisho itaonekana kuwa na dosari za kitaalam ambazo zitahitaji kufanyiwa marekebisho.
  • Kuwa na uhakika kuhusu mahitaji muhimu ya kuzingatiwa wakati michoro inaandaliwa.

3. JINSI YA KUWASILISHA MAOMBI YA KIBALI CHA UJENZI

  • Baada ya michoro kukamilika, iwasilishwe ikiwa kwenye majalada kwa namna ambayo inaweza kufunguliwa na kusomeka michoro hiyo iwasilishwe kama ifuatavyo:-
  • Seti tatu za michoro ya jengo (Architectural drawings scale 1:100 & 1:50)
  • Seti mbili za michoro ya vyuma structural drawings (scale 1:50) kwa majengo ya ghorofa.

4. MICHORO ILIYOANDALIWA IONYESHE NINI:

Michoro itakayoandaliwa inatakiwa ionyeshe mambo yafuatayo:-

  • Namna jengo litalavyokuwa ”sections elevation”, "foundation”, “roof plan”, “site plan”.
  • Ramani ya kiwanja (location plan)
  • Namba na eneo la kiwanja kilipo
  • Jina la mmilikaji ardhi inayohusika
  • Jina la mchoraji, ujuzi na anwani
  • Ukubwa wa kiwanja kwa mita za mita za mraba
  • Ukubwa wa jengo kwa mita za mraba
  • Ujazo wa kiwanja (plot coverage).
  • Uwiano (Plot ratio)
  • Urefu wa jengo kwenda juu (Height)
  • Matumizi yanayokusudiwa
  • Idadi ya maegesho yatayokuwepo
  • Umbali wa jengo kutoka kwenye mipaka ya kiwanja (setbacks) na
  • Mfumo wa kutoa maji taka hadi kwenye mashimo, au bomba la maji taka

5. VIAMBATANISHO:

  • Fomu moja ya maombi iliyojazwa kwa usahihi.
  • Hati ya kumiliki kiwanja au barua ya toleo au fomu iliyojazwa ya sehemu zisizopimwa.
  • Kumbukumbu nyingine zinazohusu kiwanja hicho kama hati za mauzo,
  • Makabidhiano n.k.
  • Nakala za risiti ya kodi ya kiwanja na kodi ya majengo.
  • Mabadiliko ya matumizi ya ardhi.
  • Ramani ya kiwanja iliyosajiliwa.

6. HATUA ZINAZOFUATWA WAKATI WA KUCHUNGUZA MAOMBI YA KIBALI

Zinafuata ni hatua zinazofuatwa wakati wa kuchunguza michoro hiyo:-

Kuwasilisha michoro na kulipia gharama ya kibali cha ujenzi.

  • Uhakiki wa miliki
  • Kukaguliwa usanifu wa michoro
  • Kukagua kiwanja kinchokusudiwa kuendelezwa
  • Uchunguzi wa matumizi ya jengo na kuwepo kwa kiwanja katika ramani M/Miji (TP drawing)
  • Uchunguzi  wa Maafisa Afya
  • Uchunguzi wa  mipango ya uondoaji majitaka
  • Uchunguzi wa tahadhari za moto
  • Uchunguzi wa uimara wa jengo
  • Kuwasilisha kwenye kikao cha mipango Miji baada ya kukamilisha taratibu zote.
  • Hatimaye kuandika na kutoa kibali.

7. FAIDA ZA KUWA NA KIBALI CHA UJENZI

  • Kujenga nyumba ambayo imethibitishwa kitaalamu kuwa ni salama.
  • Kuwa na mazingira bora kwa kuwa na mji uliopangwa.
  • Kuepuka hasara na usumbufu unaoweza kutokea iwapo ujenzi umefanyika bila kibali ikiwa ni pamoja na kushtakiwa mahakamani kuvunjiwa na kulipa gharama za uvunjaji.
  • Kulipwa fidia iwapo jengo litabomolewa kwa sababu maalum.
  • Kuweza kupata mkopo kutoka Taasisi za fedha.

8. MUDA

  • Michoro itaidhinishwa ndani ya siku saba (7) toka mwombaji awasilishe maombi ya jengo la chini (mfuto). Na siku kumi nne (14) jengo la ghorofa. Aidha ndani ya muda huo mwombaji ataarifiwa sababu za michoro kutoidhinishwa kupata kibali cha ujenzi.

SOURCE: https://kinondonimc.go.tz/vibali-vya-ujenzi

Share This